Welcome
Mustlead Schools

Mustlead Pre & Primary School is a Private school that provides early learning, primary and Secondary education. The school is situated on a friendly and secure environment in Bagamoyo District at Masuguru Village, on the Bagamoyo to Msata Road.

SCHOOL FACILITIES

MustLead Grade 7 Results 2024

Admission For 2026

Admission Window is Now Open!

Mkuu wa shule ya Msingi na Sekondari Mustlead anawakaribisha wazazi na walezi kufanya usajili wa watoto kuelekea mwaka wa masomo 2026, Dirisha la usajili liko wazi kuanzia Chekechea hadi kidato cha tatu, Shule ni ya kutwa na bweni, jinsia zote (Wavulana na Wasichana) Shule ipo Masuguru, Pembezoni mwa barabara ya Bagamoyo-Msata Mkoani Pwani, Nyote Mnakaribishwa!

Mustlead (Pre & Primary) - Love Learn Lead.

Mustlead (Secondary) - Aspire Action Attain.

Welcome to Our Dar es salaam Branch

Moriah Daycare.

Bunju, Dar es salaam.

+255 769 522 222

+255 786 202 202

Why choose MUSTLEAD?

Mustlead Schools offers students a supportive and future oriented learning environment sustained by quality teachers, experienced staff and modern, well-resourced facilities. Our teachers are committed to the provision of a relevant education, which incorporates the best of traditional, well-proven techniques with up-to-date, modern practices and resources. The staff and community of this school seek to achieve, in our students, strong personal development where children are encouraged to be responsible, caring and productive citizens.

Our Core Values

Kibubu cha Ada

Karibu shule za Mustlead kuanzisha kibubu chako kuelekea mwaka wa Masomo 2025, Kibubu cha ada kitakuwezesha mzazi/mlezi kuweka akiba kidogo kidogo kwenye Kibubu cha Ada ili kulipia Ada muda wa masomo utakapoanza, Wengi walioweka akiba kwenye kibubu cha ada mwaka jana wamenufaika na kusomesha watoto wao bila shida, 

Kujua zaidi kuhusu Kibubu cha ada kutoka shule za Mustlead usisite kuwasiliana nasi kwa namba 0676 668 589 kwa shule ya Msingi au 0713150841 au kwa email info@mustleadschools.ac.tz

MustLead, Ni yetu Sote.

 

Sababu 20 Kwa Nini Mwanao Asome Shule za MustLead

1. Mfumo wa Ada
Mfumo wa malipo ya ada ni chaguo la mzazi. Unapanga ulipe ada kwa awamu ngapi. Unaweza kulipa kwa awamu 1,2,3,4,5,6,7,8,9 au 10. Unaweza kulipa ada kwa kila wiki pia. Unachagua wewe.
2. Masomo ya Ziada
Wanafunzi wanafundishwa pia Maarifa ya ziada mf. Kompyuta, Kilimo-Biashara (Matunda na Mboga Mboga), Ufugaji, Sanaa na Michezo n.k.
3. Lugha za Kigeni
Tunafundisha lugha za Kigeni mf. Kifaransa, Kichina na Kiingereza. Lugha hizi ni muhimu katika karne hii ya utandawazi.
4. Fedha na Vipaji
Wanajifunza Maarifa ya fedha na Maisha, Utambuzi wa Vipaji, Ujasiriamali n.k ili wakimaliza shule waweze kujiajiri.
5. Mfumo wa Malipo
Mfumo wa malipo umerahisishwa kweli kweli. Mzazi analipa ada popote alipo na wakati wowote kwa kutumia namba maalumu ya mwanafunzi ya malipo (Control Number) akiwa Bank, Kwa Wakala au Kupitia Simu yake ya Mkononi.
6. Taarifa za Mwanafunzi
Mzazi anapokea taarifa za Maendeleo ya mwanafunzi kitaaluma Mf. Majaribio na mitihani ya kila mwezi kupitia simu yake ya mkononi (App) popote alipo. Hivyo kupunguza usumbufu kwa mzazi.
7. Taaluma
Shule inafanya vizuri Kitaifa, Kimkoa na Kiwilaya. Mwaka 2020 ilishika nafasi ya kwanza matokeo ya darasa la saba Kiwilaya katika kundi lake.
8. Kibubu cha Elimu
Mustlead Schools ni shule pekee nchini ambapo kuna mfumo maalumu kwa wazazi wenye kipato kidogo na kisicho na uhakika. Unalipa ada kidogo kidogo kabla ya mhula kuanza au ndani ya mhula. Unaweka kiasi cha fedha yoyote unayopata kwenye kibubu chako unacho-tengenezewa na shule. Utapatiwa risiti ya mashine (EFD) kila unapoweka fedha.
9. Mazingira
Mazingira ya kusoma ni mazuri. Zipo sehemu za wazi wanafunzi kusoma na kufanya mijadala. Shule imejitenga sehemu ya utulivu. Ulinzi niwauhakika.
10. Dini na Maadili
Kila mwanafunzi anapata muda wa kushiriki ibada kwa imani na dhehebu lake. Siku za ibada, Magari ya shule huwapeleka wanafunzi, Waislam Msikitini Siku ya Ijumaa. Wakristo hupelekwa kanisani Wakiwa na walimu wao. Walimu wanasimamia maadili ibasavyo.
11. Wafanyakazi wa Pekee
Shule inawafanyakazi wenye Upendo. Watiifu na Waadilifu. Wabunifu na Wachapa kazi, ambao wanaishi ndani ya eneo la shule. Zipo nyumba za walimu.
12. Afya
Huduma za Afya, Maji na Chakula zimepewa umuhimu wa kutosha. Wapo Waalimu Wanao simamia afya za wanafunzi. Ipo Zahanati ya karibu. Kuna gari la shule kwa ajili ya wagonjwa masaa 24.
13. Michezo
Kuna viwanja vya michezo. Wanafunzi kupitia walimu wa michezo hufanya mazoezi na kushiriki katika mashindano mbalimbali ya UMITASHUMTA na UMISETA. Baadhi ya wanafunzi wamefika hadi ngazi ya mkoa katika mashindano mbalimbali ya michezo.
14. Kutembelea Wanafunzi
Kwa wanafunzi wa Bweni, Kila Jumamosi ya Mwisho wa mwezi mzazi anaruhusiwa (akipenda) kumtembelea mtoto shuleni. Hii hutoa fursa kwa wazazi kuwaona watoto wao kutegemeana na muda wao.
15. Ofa Mbalimbali
Wenye mtoto zaidi ya mmoja hupewa punguzo la asilimia 5 (5% off) ya ada. Waliomaliza elimu ya msingi hapa kwetu (Mustlead Primary School) na kujiunga na shule ya Sekondari ya MUSTLEAD hupewa punguzo la asilimia 10 ya ada (10% off).
16. Kujiunga ni Rahisi
Piga simu ya shule 0753 211 111 kwa shule ya Msingi na 0713 150 841 kwa shule ya Sekondari. Aidha, Fomu za Kujiunga unaweza kutumiwa kwa njia ya Mtandao au ukafika shuleni moja kwa moja. Unaweza pia kutembelea tovuti yetu (www.mustleadschools.ac.tz)
17. Bweni
Huduma za Bweni ni za Kiwango cha juu. Wanafunzi hulala kulingana na umri na jinsia. Kila Bweni lina walezi wawili kuwahudumia watoto. Aidha, watoto hupewa mafunzo ya maisha ya nyumbani na maadili.
18. Zawadi kwa Wahitimu
Kila mwaka shule hutoa zawadi kwa wahitimu, ikiwemo Tshirts na Vitabu Vya Maarifa Mbalimbali. Vitabu vilivyotolewa kwa wahitimu hadi sasa ni TETEMEKO LA UJANA (2020), KIJANA MWENYE NDOTO KUBWA (2021) na WHY YOU SHOULD NOT LOSE HOPE (2022).
19. Tuzo
Taasisi imepokea Tuzo mbalimbali za Ushindi. Moja ya Tuzo Kubwa ni ile ya Ushindi wa Shindano la Ujasiriamali Nchini kutoka Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC). Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa alikabidhi zawadi hizo kwa MUST LEAD
20. Usafiri wa Uhakika
Wanafunzi wa Kutwa huchukuliwa na kurudishwa na gari za shule. Barabara ya Chalinze-Msata, Bagamoyo-Msata, Tanga-Msata gari za shule hupita. Ndani ya kila gari kuna Mwalimu-Msimamizi kwa Usalama wa Watoto. Madereva wa MUST LEAD ni Nadhifu sana na Makini wakati wote.

OUR VISION AND MISSION

Mustlead Schools - Vision & Mission

Vision

To graduate competent and self-reliant students who cope well with contemporary local and global market for their socio-economic prosperity.

Mission

To adopt national education curriculum and capitalize on power of network, digital platform and collaboration with local and international likeminded partners.

Time to remember...

Study Tour 2023

Our Powerful Staff

Form 4 Graduation 2025

5th Grade 7 Graduation

Mustlead Schools Team

Contact Us

[fluentform id="1"]
Bar Text Slider
ADMISSIONS OPEN!
Mustlead Pre, Primary & Secondary School is now enrolling for academic year 2026
Admission forms are available at...
Mustlead Main branch [Masuguru, Bagamoyo - Msata road, Pwani]
Mustlead Lugoba Branch [Lugoba, Chalinze - Tanga road]
Mustlead Kiwangwa Branch [Kiwangwa, Bagamoyo, Pwani]
Mustlead Msata Branch [Msata, Junction to Chalinze, Bagamoyo and Tanga]
Forms are also available at Moriah Daycare and Preschool [Bunju, Dar es salaam]
You are all warmly welcome
Perfect Replica Watches UK ‣ The Best Swiss Made 1:1 Replica Rolex Watches « Store:perfectreplica.cc. Best AAA hublot Replica Watches UK – Buy Cheap Fake Hublot For Sale:hublotcopy.com. TAG Heuer Top Replica Rolex Watches Site – Best Replica Watches UK:tagheuerreplica.com.